In Summary
  • Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Ephraim Kwisegabo alisema hayo alipokuwa akitoa taarifa ya mfumko wa bei kwa mwezi uliopita.

Mfumuko wa bei umeongezeka kwa asilimia 0.1 mwaka 2017 kutoka wastani wa asilimia 5.2 wa mwaka 2016 hadi asilimia 5.3.

Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Ephraim Kwisegabo alisema hayo alipokuwa akitoa taarifa ya mfumko wa bei kwa mwezi uliopita.

“Kuna mabadiliko madogo ya wastani wa mfumuko wa bei kwa mwaka 2017 ikilinganishwa na mwaka 2016. Vyakula vinachangia kwa asilimia 38.5 hivyo bei zake zikibadilika sana kuna uwezekano wa mfumuko wa bei kwa kipindi husika ukayumba,” alisema Kwisegabo.