In Summary

“Sikuwa nafahamu kuna bahati nasibu inayochezwa na benki. Niliweka fedha katika akaunti yangu kama kawaida. Nilishangaa maofisa wa benki waliponipigia simu na kunieleza kuwa ni mshindi,” alisema.

Dar es Salaam. Mchungaji wa Kanisa la FPCT la Kurasini wilayani Temeke, Reuben Kinamhala ameshinda Sh10 milioni kutoka Benki ya Afrika (Boa). Aliibuka mshindi wa kampeni ya daka mkwanja iliyokuwa inachezwa na benki hiyo ili kuhamasisha wateja wake kujiwekea akiba.

“Sikuwa nafahamu kuna bahati nasibu inayochezwa na benki. Niliweka fedha katika akaunti yangu kama kawaida. Nilishangaa maofisa wa benki waliponipigia simu na kunieleza kuwa ni mshindi,” alisema.

Naye meneja masoko, utafiti na maendeleo wa Boa Tanzania, Muganyizi Bisheko alisema kampeni hiyo ya miezi minne ilianza Novemba mwaka jana na washiriki walitakiwa kuweka kiwango kisichopungua Sh1 milioni kwenye akaunti zao.