In Summary
  • Tuzo hiyo imetolewa na Taasisi ya Africa Invest (Ai) jijini New York, Marekani kwenye mkutano¬† wa tisa wa kutambua mchango wa masoko ya mitaji katika ukuzaji wa uchumi wa mataifa husika.

Dar es Salaam. Mamlaka ya Soko ya Mitaji na Amana (CMSA) nchini imetunukiwa tuzo ya ubunifu Afrika kwa mwaka 2016.

Tuzo hiyo imetolewa na Taasisi ya Africa Invest (Ai) jijini New York, Marekani kwenye mkutano  wa tisa wa kutambua mchango wa masoko ya mitaji katika ukuzaji wa uchumi wa mataifa husika.

Meneja Mawasiliano wa CMSA, Charles Shirima amesema ushindi huo ulipatikana baada ya kuwa mamlaka ya kwanza kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati kutumia simu za mkononi kununua na kuuza bidhaa za soko la hisa.