In Summary

Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Apili Mbaruku amesema hayo jana wakatia akikabidhi lita 8,180 za mafuta ya taa yenye thamani ya Sh4.9 milioni kwa Jeshi la Magereza. 

Arusha. Bidhaa zenye thamani ya Sh568.1 milioni zilizoingizwa kwa njia ya magendo mkoani Arusha kuanzia Januari hadi Septemba mwaka huu, zimekamatwa.

Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Apili Mbaruku amesema hayo wakatia akikabidhi lita 8,180 za mafuta ya taa yenye thamani ya Sh4.9 milioni kwa Jeshi la Magereza. Mbaruku amesema kutokana na bidhaa za magendo, TRA imekusanya Sh 236.2 milioni zikiwa ni kodi kwa kipindi hicho.

Akipokea msaada huo kwa niaba ya Mkuu wa Gereza Kuu la Arusha, Inspekta Sylvester Sangida amesema mafuta hayo yatatumika pindi  umeme utakapokatika katika Magereza ya Loliondo na Mang’ola na Arusha.