In Summary
  • Ni katika kusherehekea wiki ya huduma kwa wateja
  • Wateja kupata GB 2 na kifurushi cha Sh1,000

 

 Wateja wa kamouni ya simu za mkononi ya airtel wamepoatiwa ofa inayohusisha kifurushi kipya chas Sh1,000 pamoja na muda wa maongezi na ujumbe mfupi kama sehemu ya maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja.

Taarifa iliyotolewa na kampuni hiyo inaeleza kuwa kifurushi hicho kitadumu kwa muda wa siku tatu.

Aidha, taarifa hiyo imeeleza kuwa wateja wakaoingia kwenye maduka ya kampuni hiyo pia watapata fursa ya kukata keki.

Wiki ya huduma kwa wateja huadhimishwa duniani kpote kati ya Oktoba 2 na 6.

Akiongea katika makao makuu ya Airtel, Meneja wa Duka la Airtel, Celine Njunju alisema: “Tunawashukuru wateja na wananchi wote kwa ujumla na ndio maana katika wiki hii ya huduma kwa wateja tutawapatia kifurushi cha ofs kabambe kupitia  Airtel Money kitakachokupa uhuru wa kujichagulia kile unachokipenda kutoka.”

Taarifa hiyo inasema kuwa mteja atakayejiunga na ofa hiyo ya Airtel Money kwa Sh1,000 atapata GB mnili za intaneti, dakika 110 za kupiga mitandao yote na SMS bila ya kikomo.

“Mwaka huu Airtel tumeipa wiki hii kauli mbiu ya ‘Building Trust’ tukimaanisha kuendelea kuwajengea wateja wote imani katika huduma tunazotoa,” aliongezaa Lyamba.