In Summary

Wananchi wameanza kujitokeza kupiga kura kwenye uchaguzi wa marudio ya ubunge jimbo la Longido Mkoa wa Arusha.

ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT

Longido. Wananchi wameanza kujitokeza kupiga kura kwenye uchaguzi wa marudio ya ubunge jimbo la Longido Mkoa wa Arusha.

Idadi ya asubuhi wakati vituo vinafunguliwa haikuwa kubwa lakini baadaye wameanza kufika kwenye vituo ambavyo havina misururu ya wapiga kura.

Msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Longido, Jumaa Mhina amesema upigaji kura umeanza vizuri na anaendelea kukagua vituo mbalimbali.