In Summary
  • Kwa kutumia M-Pesa unaepuka uwezekano wa kupewa noti bandia, kupoteza fedha au kuibiwa.

Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom kuelekea msimu wa sikukuu za mwishoni mwa mwaka inawazawadia wateja wake fedha, muda wa maongezi na MB.

Vodacom inatoa zawadi hizo kwa watumiaji wa M-Pesa wanaoitumia kufanya ununuzi.

Kampuni hiyo Novemba 30,2017 imezindua kampeni inayojulikana ‘Pesa ni M-Pesa’ ambayo itawawezesha watumiaji wa M-Pesa katika kufanya malipo ya huduma na bidhaa kupata zawadi hizo.

Taarifa ya Vodacom imesema kwa zawadi ya fedha, zitaingizwa kwenye akaunti za M-Pesa.

“Wakati tukifurahia msimu wa sikukuu ambapo watu wengi hufanya ununuzi, Vodacom itakuwa ikiwazawadia wateja wake fedha wanapolipa kwa kutumia M-Pesa,” amesema Sitoyo Lopokoiyit, mkurugenzi wa biashara kwa mtandao wa Vodacom.

Amesema kampeni hiyo inayofanyika nchi nzima inalenga kuongeza uelewa kwa umma kuhusu urahisi wa kulipa kwa kutumia M-Pesa.

“Tunataka wateja wajue kuwa, kulipa kwa M-Pesa ni rahisi na salama. Huhitaji kubeba burungutu la fedha unapokwenda kufanya ununuzi. M-Pesa inasaidia kuokoa muda wa kwenda kwenye ATM au kupanga foleni benki,” amesema Lopokoiyit.

Akizungumzia urahisi wa huduma ya M-Pesa meneja masoko na biashara kwa mtandao wa Vodacom, Noel Mazoya amesema, “Kwa kutumia M-Pesa unaepuka uwezekano wa kupewa noti bandia, kupoteza fedha au kuibiwa.”

Mwisho.