In Summary
  • Kiongozi wa timu ya DFID, Getrude Mapunda akizungumza kwenye mkutano wa uzinduzi wa mradi huo ambao ni wa tatu na unaosimamiwa na Tume Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), amesema wameongeza fedha hizo baada ya kuridhishwa na miradi mingine iliyopita.

 Serikali ya Uingereza kupitia Shirika la Maendeleo (DFID), imeongeza ufadhili wa Pauni  10 Milioni sawa  na Sh28 milioni kwa ajili ya kusaidia miradi ya ubunifu na teknolojia mbalimbali nchini, ikiwamo malezi bora ya watoto.

Kiongozi wa timu ya DFID, Getrude Mapunda akizungumza kwenye mkutano wa uzinduzi wa mradi huo ambao ni wa tatu na unaosimamiwa na Tume Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), amesema wameongeza fedha hizo baada ya kuridhishwa na miradi mingine iliyopita.

Mkurugenzi wa COSTECH, Dk. Hassan Mshinda alisema wamefurahi kuongezeka kwa fedha hizo kwa kuwa zinatoa nasafi miradi ya ubunifu na yenye kuleta maendeleo kufanyika hivyo kusaidia nchi kufikia  kwenye maendeleo kwa nyanja mbalimbali ikiwamo afya na elimu.

"Tume imekuwa nchini kutokana ushindani wa uwekezaji kuwa mkubwa kwa kusaidia katika kutekeleza na kuendeleza tafiti na maendeleo ya teknolojia nchini, kama mradi huu wa watoto utasaidia katika kutoka muongozo mzuri katika ukuaji wao kwenye afya na elimu," anasema Dk Mshinda.