In Summary

Omolo hayuko peke yake. Wakulima wengi wadogo wa wilaya hii wanakabiliwa na kipindi kigumu cha miezi minne ya ukame kila mwaka. Hakuweza kukabiliana na hali hiyo hadi alipokutana na mkulima mwenye utaalamu aliopewa na taasisi ya Aga Khan Foundation (AKF). Hapo alijifunza kilimo endelevu na kuongeza uzalishaji.

Kwa miaka mingi Athumani Mohamed Omolo, mkulima mdogo wa Mtwara Vijijini hakuweza kuzalisha vya kutosha ili kuilisha familia yake.

Omolo hayuko peke yake. Wakulima wengi wadogo wa wilaya hii wanakabiliwa na kipindi kigumu cha miezi minne ya ukame kila mwaka. Hakuweza kukabiliana na hali hiyo hadi alipokutana na mkulima mwenye utaalamu aliopewa na taasisi ya Aga Khan Foundation (AKF). Hapo alijifunza kilimo endelevu na kuongeza uzalishaji.

“Maisha yangu sasa si mabaya, iwe ni wakati wa ukame au wa mvua. Kwa kutumia kilimo cha mbogamboga, naweza kukabiliana na hali ya umaskini na sasa ninaweza kuhudumia familia yangu,” anasema Omolo.

Anasema mabadiliko hayo katika maisha yake yanatokana na kujifunza kilimo cha bustani ambacho kimemuongezea uzalishaji na uuzaji mbogamboga. Leo hii Omolo si tu anaweza kuihudumia familia yake, bali pia analipa ada za shule kwa kutumia kipato kinachotokana na kilimo.

Wakulima wadogo wa mikoa ya Mtwara na Lindi wamekuwa na historia ndefu ya vikwazo dhidi ya kilimo cha kibiashara, vikwazo ambavyo ni matokeo ya changamoto tofauti zinazohusu uzalishaji na masoko. Moja ya malengo ya AKF imekuwa ni kuwasaidia wakulima kama Omolo kujifunza uzalishaji endelevu unaozingatia ubora ili kumudu ushindani uliopo katika soko la kilimo.

Tangu mwaka 2009, AKF imewafikia wakulima zaidi ya 100,000 katika mikoa ya Lindi na Mtwara kwa njia ya mifumo mbalimbali, kuwezesha upatikanaji wa pembejeo za ubora, habari na taarifa kuhusu kilimo bora na ushirikiano wa soko.

Mikoa hii kwa sasa inashuhudia mabadiliko ya taratibu kutoka uzalishaji duni, usio na mpangilio na wa kujitosheleza kwa chakula kwenda katika uzalishaji endelevu unaozingatia soko.

Hii imechangia kuongezeka kwa mavuno, mapato, kuweka akiba, usalama wa chakula na ukuaji wa biashara ndogo ndogo hasa miongoni mwa wajasiriamali wa ndani, wakiwemo wanawake na vijana. Wakulima walengwa wameongeza mavuno na mapato, wakati usalama wa chakula umeongezeka.

Mwaka 2014 asilimia 60 ya kaya zilitajwa kuwa na usalama wa chakula ikilinganishwa na asilimia 27 ya mwaka 2010 katika maeneo ya mradi.

Makampuni madogo na ya kati zaidi ya 200 yanayojishughulisha na biashara inayohusiana na kilimo yanasaidiwa na AKF ili kukuza biashara zao. Kwa kufanya kazi katika njia tofauti zinazoongeza thamani ya bidhaa (kilimo cha mbogamboga, mchele, kunde, alizeti, ufuta na uzalishaji vifaranga), AKF inawezesha wakulima kuzalisha na kupata masoko ya mazao mchanganyiko ili kusaidia kupunguza athari za kushuka kwa bei au kutopata mazao.

Pia kusaidia kukusanya pamoja watu tofauti kutoka sekta binafsi. Mbinu ya uimarishaji mifumo kwa ushirikiano na wadau muhimu hutumika katika kila hatua ya mchakato wa uongezaji thamani ya mazao ya kilimo.

AKF - wakala wa Mtandao wa Maendeleo wa Aga Khan inachukua mbinu ya muda mrefu inayojumuisha sekta tofauti kuboresha maisha katika jamii ambayo inafanya kazi. Ili kufikia lengo hili, AKF inashirikiana na wadau wengine na inakusanya pamoja rasilimali za kibinadamu, za kifedha na za kiufundi zinazohitajika kuimarisha taasisi na mifumo mbalimbali.

AKF imejenga uaminifu na serikali za mitaa, jamii na sekta binafsi. Hii ni muhimu kwa jukumu lake kama mwekezaji wa kuaminika wa soko.

Usaidizi wa upanuzi wa kilimo

Uwezo wa kupata pembejeo zenye ubora na teknolojia muafaka umekuwa duni katika mikoa ya Lindi na Mtwara kutokana na masuala ya uhitaji na ugavi.

AKF iliamsha mahitaji ya nafaka, dawa, pembejeo sahihi na teknolojia endelevu na isiyoharibu mazingira (pampu za mikono, umwagiliaji usiotumia maji mengi na nyumba za mazao ya mbogamboga) kwa kuhamasisha tabia ya kilimo bora kwa wakulima, kuwezesha mashamba ya mfano pamoja na ziara za kubadilishana uzoefu.

Hatua hii ilisaidia wakulima kuongeza uzalishaji na ongezeko la mahitaji ya pembejeo hizo na teknolojia. Wakati huohuo, chini ya programu ya ujasiriamali, AKF ilitoa mafunzo kwa mawakala 257 wanaofanya kazi katika vijiji (VBAs) na kati yao 177 sasa wanaendesha biashara ya pembejeo za kilimo, hivyo kuunganisha hadi hatua ya mwisho pembejeo na teknolojia. AKF iliunganisha VBA na kampuni zinazosambaza pembejeo na teknolojia hizo ambazo hazikuwa zikifanya kazi maeneo hayo.

“Awali nililazimika kusafiri kwa hadi saa moja kwenda Masasi mjini au kumuomba mtu anayesafiri kutoka Mtwara kwenda Dar es Salaam kuninunulia mbegu bora na pembejeo ambazo sikuweza kupata kutoka hapa, kitu ambacho kiligharimu fedha nyingi na kuchukua muda mrefu,” anasema Devota Chigungu.

“Lakini siku hizi zinapatikana sehemu inayoweza kufikika kwa kutumia VBA waliopewa mafunzo na AKF. Pia wanakushauri jinsi ya kutumia pembejeo.”

Usimamizi baada ya mavuno

Uhifadhi bora, upangaji wa madaraja, uchambuaji na uchakataji wa mazao unaongeza ushindani kwa kupunguza hasara, kuongeza ubora na thamani.

AKF imeshirikiana na vyama vya wakulima, wasagaji, serikali za mitaa na vyama vya wanunuzi katika maeneo tofauti ya mikakati kuboresha usimamizi wa mazao baada ya mavuno. Hii ni pamoja na mafunzo ya kuvuna wakati sahihi, kuboresha uhifadhi na vifaa vya usagaji, kuhimiza uchambuzi na uwekaji katika madaraja, ujenzi au ukarabati wa maeneo ya kuhifadhia na miundombinu ya masoko.

Katika ushirikiano wa Serikali na sekta binafsi (PPP) na Halmashauri ya Wilaya ya Masasi na chama cha soko la ndani, AKF iliwezesha ujenzi wa kituo cha kukusanyia mazao ya mbogamboga ambacho kinamilikiwa na kuendeshwa na wanajamii kwa ajili ya kuhifadhia mbogamboga katika Kijiji cha Chidya mwaka 2017.

Kituo hicho kinawezesha mazao yatokanayo na kilimo cha bustani, kuhifadhiwa katika vyumba vya ukavu na ubaridi, matumizi ya mizani yenye vipimo sahihi na imesaidia kupunguza hasara na kudhibiti wizi huku kikiwavutia wanunuzi wengi zaidi.

“Awali, tulikuwa tunategemea wanunuzi haohao kila wakati na tulipokata tamaa ya kuuza, tulilazimika kukubaliana na hali yoyote iliyowekwa na mnunuzi, ikiwa ni pamoja na kununua kwa mkopo,” alisema Said Athuman ambaye anauza mbogamboga katika soko la Chidya.

“Wakati huu ambao kuna kituo, kama mnunuzi hana pesa ya kulipa, wakulima wanayo fursa ya kuuza kwa mtu mwingine. Na kwa hiyo hakuna tena ucheleweshaji mkubwa katika kupata malipo ya haki wanayostahili.”

Tangu kuanzishwa kwake, kituo hicho kimewanufaisha wakulima zaidi ya 800 wa Chidya na kijiji cha jirani cha Chiwata, na imechangia mabadiliko ya muda mrefu ya mfumo wa soko la ndani kwa ajili ya manufaa ya wakulima wa maeneo hayo.

Upatikanaji rahisi wa fedha

Jitihada za AKF katika kuongeza upatikanaji wa fedha za msingi kwa njia ya kikundi cha akiba ya jamii (CBSG) zimefikia wanachama zaidi ya 180,000 huku asilimia 66 wakiwa wanawake.

Kwa kuandaliwa katika makundi zaidi ya 9,300, wanawake na wanaume katika maeneo ya vijijini wanaokoa wastani wa Sh200,000 kwa kila mtu kila mwaka, na makundi haya yanaokoa kwa kiasi kikubwa Sh33 bilioni kwa mwaka (karibu dola milioni 15).

Uwezo huo wa wakulima katika kuboresha kilimo pamoja na ushiriki wao katika CBSG umewapatia fursa ya kuweka akiba, mikopo na uwekezaji katika elimu ya watoto, afya ya familia, biashara, na ununuzi wa pembejeo na huduma za kilimo, na kusababisha ustawi mkubwa, uzalishaji na ubora wa maisha.

Kujenga mafanikio haya, AKF inaendesha jukwaa la ubunifu la simu za mkononi pamoja na kampuni ya teknolojia ili kuwawezesha wanachama wa hifadhi, hasa katika maeneo ya vijijini, kuokoa na kukopa kwa kutumia simu zao za mkononi.

Kuunganisha wadau sokoni

Mbinu mbalimbali zilizofanywa na AKF zimechangia kukua kwa masoko ya bidhaa za kilimo katika mikoa ya Lindi na Mtwara. Hii ni pamoja na kuboresha mtiririko wa habari kati ya wakulima na masoko, mafunzo ya wakulima juu ya kilimo kama biashara, na kuhamasisha vikundi vya mifano (makundi ya biashara ya wakulima, vyama vya ushirika wa msingi, kilimo cha mikataba na kuboresha miundombinu ya soko na kuhifadhi) ili kuvutia na kuwakusanya wengi zaidi katika sekta binafsi na kuwezesha uchumi wa kiwango.

Kiashiria kimoja cha kukua kwa masoko katika mikoa ni idadi kubwa ya makampuni ya biashara ya binafsi na kuongeza kiasi cha shughuli za biashara kati ya wanunuzi na wazalishaji hasa wa mchele, mboga, na sesame.

Aga Khan Foundation, Shirika la Aga Khan Development Network, ni shirika la kibinafsi, lisilo la kibiashara, lisilo la kidini la kimataifa ambalo limeanzishwa na Mtukufu Aga Khan.