In Summary
  • Mamlaka za Rwanda zinawashutumu kina Rwigara kwa ukwepaji kodi na huenda jengo la kifahari lililopo eneo la Kiyovu, Kigali likaorodheshwa kuwa miongoni mwa mali za kukamatwa katika kipindi cha wiki mbili zijazo, ikiwa ni nyongeza kwa kampuni ya sigara ya Premier Tobacco, ardhi, magari na mali nyingine.

Familia ya Rwigara iliyokuwa na ukwasi mkubwa wa mali nchini, siku chache zijazo huenda ikajikuta haina makazi ikiwa mamlaka zitaendelea na mpango wa kupiga mnada mali zao ili kupata faranga 5 bilioni (dola za Marekani 6 milioni) inazodaiwa.

Mamlaka za Rwanda zinawashutumu kina Rwigara kwa ukwepaji kodi na huenda jengo la kifahari lililopo eneo la Kiyovu, Kigali likaorodheshwa kuwa miongoni mwa mali za kukamatwa katika kipindi cha wiki mbili zijazo, ikiwa ni nyongeza kwa kampuni ya sigara ya Premier Tobacco, ardhi, magari na mali nyingine.

"Ikiwa watashindwa kulipa kodi hadi mwishoni mwa Novemba, tutaanza kuweka mali zao kwenye mnada," amesema Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kodi ya Rwanda (RRA), Richard Tusabe.

Tusabe aliongeza kwamba mnada huo utasitishwa tu ikiwa akina Rwigara watakuja hapa na mpango unaoeleweka wa kulipa deni.

Vyanzo kutoka ndani ya sekta ya fedha vimeliambia gazeti la The EastAfrican kwamba benki zilizoikopesha familia ya Rwigara zinatarajia kukamata mali za familia hiyo na kuziuza kwa mnada.

Lakini familia hiyo imesisitiza kwamba mashtaka dhidi yao yamechochewa kisiasa na yana lengo la kuwanyamazisha ili wasiendelee kuikosoa na hivyo kuwafilisi.

Katika kikao cha mahakama mwezi uliopita, mwakilishi wa familia hiyo ya wafanyabiashara Anne Rwigara, dada wa Diane Rwigara aliyekosa sifa za kugombea urais Agosti, aliwaambia majaji kuwa maofisa wa mamlaka ya mapato walijaribu kumlazimisha kutia saini mpango wa malipo ambayo aliona ni vigumu kutekeleza.

Title>>>>>>>>>>>>>>Serikali, mabenki kupiga mnada mali za Rwigara

Kigali, Rwanda. Familia ya Rwigara iliyokuwa na ukwasi mkubwa wa mali nchini, siku chache zijazo huenda ikajikuta haina makazi ikiwa mamlaka zitaendelea na mpango wa kupiga mnada mali zao ili kupata faranga 5 bilioni (dola za Marekani 6 milioni) inazodaiwa.