In Summary

Rashford alipata majeraha ya goti 

London, England. Kocha wa England, Gareth Southgate, amesema ana matumaini mshambuliaji wake kinda Marcus Rashford ataikabili Tunisia.

Rashford alipata majeraha ya goti na kuibua hofu kwa kocha Southgate kama atacheza kwa ufanisi fainali hizo zinazoanza leo nchini Russia.

Mchezaji huyo alikosa mazoezi ya kwanza katika kikosi cha England, lakini kocha huyo alisema ana matumaini nyota atacheza mchezo dhidi ya Tunisia.

Kiungo wa pembeni, Raheem Sterling anatarajiwa kuanza katika kikosi hicho akicheza pacha na nahodha wake Harry Kane katika safu ya ushambuliaji.

Sterling, anaweza kucheza kwa kiwango bora licha ya jana kugongana na Eric Dier, katika mazoezi ya kikosi hicho.