In Summary
  • Taarifa ya Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Gerson Msigwa, iliyotolewa leo (Jumatatu) kwa vyombo vya habari imesema katika ziara hiyo, Rais atazindua viwanda vikubwa vitano.

 Rais John Magufuli kesho (Jumanne) anaanza ziara ya kikazi ya siku tatu mkoani Pwani.

Taarifa ya Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Gerson Msigwa, iliyotolewa leo (Jumatatu) kwa vyombo vya habari imesema katika ziara hiyo, Rais atazindua viwanda vikubwa vitano.

Viwanda hivyo vimetajwa kuwa ni cha vifungashio (Global Packaging Co. Ltd), cha matrekta (Ursus- Tamco Co. Ltd), cha chuma (Kiluwa Steel Group), cha kukausha matunda (Elven Agric Company) na cha vinywaji baridi (Sayona Fruits).

Msigwa amesema Rais pia atazindua mradi wa maji wa Ruvu na Barabara ya Bagamoyo- Msata.

Taarifa imesema Rais Magufuli katika ziara hiyo atakutana na kuzungumza na wananchi katika mikutano ya hadhara iliyoandaliwa.

Mwisho.