In Summary
  • Ni mara yake ya pili kuja Tanzania

 Rais wa Rwanda, Paul Kagame amewasili  nchini leo Jumapili, Januari 14 kwa ziara ya siku moja.

Rais Kagame aliyepokewa na mwenyeji wake Rais John Magufuli,  baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius  Nyerere (JNIA) alielekea katika chumba maalum na kukaa kwa takribani dakika 30.

Aliondoka uwanjani hapo saa 4:47 asubuhi kuelekea Ikulu ambako atafanya mazungumzo na Rais Magufuli.

Hii ni mara ya pili kwa rais huyo kutembelea Tanzania tangu mwaka 2015,  mara ya kwanza ilikuwa mwaka 2016 ambako alishiriki maonyesho ya 40 ya kimataifa ya biashara (sabasaba).