In Summary

Juzi katika mitandao ya kijamii zilisambaa taarifa za kufariki kwa mwanasiasa huyo lakini muda mfupi baadaye Mrema alikanusha akisema ni mzima wa afya njema.

Dar es Salaam. Mwenyekiti wa TLP, Augustine Mrema leo Ijumaa ametoa taarifa za kuzushiwa kifo katika Kituo cha Polisi cha Oysterbay wilayani Kinondoni ili wahusika waweze kuchukuliwa hatua za kisheria.

Juzi katika mitandao ya kijamii zilisambaa taarifa za kufariki kwa mwanasiasa huyo lakini muda mfupi baadaye Mrema alikanusha akisema ni mzima wa afya njema.

Akizungumza na Mwananchi leo Ijumaa, Mrema amesema yupo Oysterbay kutoa taarifa ili suala hilo lichunguzwe na Jeshi la Polisi ili wamnase aliyesambaza taarifa hizo.

“Nipo Oysterbay Polisi namalizia taratibu za kuandikisha kesi hii, nikimaliza nitakujulisha kwa kina kuhusu suala hili,” amesema.