In Summary
  • Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, John Kauga amesema Sosopi anashikiliwa kwa kosa alilotenda Juni 16

Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha), Patrick ole Sosopi anashikiliwa na polisi kwa madai ya kufanya mkutano bila kibali.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, John Kauga amesema Sosopi anashikiliwa kwa kosa alilotenda Juni 16.

Amesema anatuhumiwa kufanya mikutano katika vijiji vya Mlowa na Kinyika vyote vilivyopo Tarafa ya Idodi wilayani Iringa pasipo kupata kibali cha jeshi hilo.

Kauga amesema kwa sasa polisi wanaendelea na uchunguzi na ukikamilika Sosopi atafikishwa mahakamani.