In Summary

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa ameshuhudia utiaji saini wa mradi huo ambao umesainiwa leo (Jumamosi) na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Bandari (TPA), Deusdedith Kakoko kwa upande wa Serikali.

Dar es Salaam. Serikali na Kampuni ya China Harbour Constructions Engineering wamesaini mkataba wa upanuzi wa kina cha mlango wa Bandari ya Dar es Salaam na katika geti namba moja hadi namba saba kwa ajili ya kuboresha na kupanua huduma zinazotolewa.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa ameshuhudia utiaji saini wa mradi huo ambao umesainiwa leo (Jumamosi) na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Bandari (TPA), Deusdedith Kakoko kwa upande wa Serikali.

Akiuzungumzia mradi huo, Profesa Mbarawa amesema gharama ya mradi ni Sh336 bilioni na utatekelezwa kwa miezi 36.

“Lakini Serikali inaendelea na mazungumzo na kampuni hiyo iliyopewa tenda ili kupunguza bei na kukamilisha mapema kabla ya muda huo uliokadiriwa awali,” amesema.