In Summary

Amehamia CCM kuunga mkono juhudi za Rais Magufuli

Iringa. Aliyekuwa Katibu wa Chadema Kanda ya Nyasa, Frenk Mwaisumbe ametangaza kuhama chama chake na kujiunga na CCM.

Mwaisumbe ambaye alishika wadhifa huo kwa kipindi cha miaka sita hadi alipoachia wadhifa huo Januari mwaka huu.

Akizungumza na wanahabari mjini hapa leo Jumatano Mwaisumbe ametaja sababu za kujiunga na CCM kuwa ni kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Rais John Magufuli za kufufua uchumi wa nchi.