In Summary

Maadhimisho hayo yanafanyika leo Ijumaa visiwani Zanzibar

Dar es Salaam. Idadi kubwa ya viongozi mbalimbali wa Serikali na wastaafu wamejitokeza kuhudhuria katika sherehe za maadhimisho ya miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar yanayofanyika sasa katika viwanja wa Amaan vilivyopo Unguja visiwani Zanzibar.

Rais wa Zanzibar, Dk Mohammed Shein anaongoza sherehe hizo akiwa sambamba na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Magufuli sambamba na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa pamoja na baadhi ya mawaziri, naibu mawaziri na wabunge mbalimbali.

Baadhi ya viongozi wastaafu waliohudhuria sherehe hizo ni pamoja na marais wastaafu akiwemo, Ali Hassan Mwinyi, Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete, Aman Abeid Karume na baadhi ya makamu wa Rais wastaafu akiwemo Mohamed Gharib Bilal.