In Summary
  • Mbunge huyo amesema inawezekana askari polisi waliohusika na sakata hilo walikuwa wanatekeleza sheria kwa maagizo ya Serikali.

Mbunge wa Kavuu, Dk Pudenciana Kikwembe amelaani kupigwa kwa walemavu waliokuwa wanaandamana wiki iliyopita jijini Dar es Salaam.

Mbunge huyo amesema inawezekana askari polisi waliohusika na sakata hilo walikuwa wanatekeleza sheria kwa maagizo ya Serikali.

"Natoa pole kwa walemavu waliopata rabsha jijini Dar es Salaam. Inawezekana ni utekelezaji wa sheria lakini si jambo jema kuwapiga walemavu," amesema Dk Kikwembe.

Amemtaka Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama kuliangalia suala hilo na kuchukua hatua zinazostahili kurekebisha makosa yatakayobainika.