In Summary

Viongozi wengine ambao hawajahojiwa hadi muda huu ni Sisya na mkurugenzi wa Idara ya sheria, Paul Kisabo.

Dar es Salaam. Mpaka kufikia leo Machi 14, 2018 saa 7:45 mchana viongozi wawili wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP) walikuwa wamekwisha hojiwa na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI).

Akizungumza na MCL Digital, ofisa habari wa mtandao huo Helleh Sisya ambaye naye pia miongoni mwa watakaohojiwa, amesema hadi muda huo waliohojiwa ni mkaguzi wa haki za binadamu , Alphonce Lusako na katibu wa mtandao huo, Malekela Brigthon.

Viongozi wengine ambao hawajahojiwa hadi muda huu ni Sisya na mkurugenzi wa Idara ya sheria, Paul Kisabo.