In Summary
  • Asasi hizo kutoka Kenya, Tanzania, Msumbiji, Uganda na Afrika Kusini zilizokutana kwa siku tatu hivi karibuni mjini Naivasha, nchini Kenya, zimekubaliana kwa kauli moja kuendelea kuupinga mradi huo wa majaribio ya mbegu za mahindi zilizobadilishwa vinasaba kwa teknolojia ya uhandisi jeni kwa kuwa teknolojia hiyo bado si rafiki na inapigiwa kelele na wadau mbalimbali katika kila kona ya dunia.

 Asasi za kiraia zinazojihusisha na utetezi na uhifadhi wa bioanuai katika nchi tano za Afrika, zimezitaka serikali za nchi zao ikiwemo Tanzania kuwa na jicho la tatu kuhusu utekelezaji wa mradi wa utafiti wa majaribio ya mbegu wa Water Efficient Maize for Africa (Wema), kutokana na mradi huo kuazungukwa na usiri kubwa.

Asasi hizo kutoka Kenya, Tanzania, Msumbiji, Uganda na Afrika Kusini zilizokutana kwa siku tatu hivi karibuni mjini Naivasha, nchini Kenya, zimekubaliana kwa kauli moja kuendelea kuupinga mradi huo wa majaribio ya mbegu za mahindi zilizobadilishwa vinasaba kwa teknolojia ya uhandisi jeni kwa kuwa teknolojia hiyo bado si rafiki na inapigiwa kelele na wadau mbalimbali katika kila kona ya dunia.

Mradi huo wa majaribio ya mbegu za Wema unaoendelea katika nchi hizi tano unajinasibu kuwa ukikamilika mbegu hizo zitakuwa suluhisho kwa kuhimili ukame, wadudu na magugu.

“Ni ukweli usiofichika kuwa mabadiliko ya tabia nchi ni changamoto inayomkabili mkulima kote barani Afrika, kadiri joto linavyoongezeka wakulima wengi wanakumbana na kadhia na madhila katika shughuli zao za kilimo, hivyo inatazamiwa kuwa mazao kama mahindi, ngano na mpunga yaweza kuathiriwa zaidi kutokana na ongezeko la joto,” inasema taarifa iliyosainiwa na Mratibu wa Tanzania Alliance for Biodiversity (Tabio) Abdallah Ramadhani Mkindi.

Mradi wa Wema ulizaliwa kutokana na changamoto hizo huku utafiti huo unaoungwa mkono na kampuni za mbegu, ukipigiwa debe na baadhi ya wasomi, lakini cha kushangaza ni pale wasomi hao wanaposhindwa kuoanisha ukweli halisi walau tu kwa yale yanayoendelea kwenye nchi ambazo awali ziliruhusu teknolojia hiyo.

Miongoni mwa nchi zinazojutia ujio wa GMO barani Afrika ni Bukinafaso ambako mwaka huu wanaendesha operesheni maalumu ya kung’oa zao lapPamba iliyobadilishwa vinasaba maarufu kitaalamu kama Bt Cotton, wakati kwa Ulaya nchi kama Ujerumani teknolojia hii imepigwa marufuku kabisa.

“Sisi asasi za kiraia kwa kauli moja, tunasema kwamba ni ukweli usiopingika kwamba tatizo la mabadiliko ya tabia nchi liko bayana kwa wakulima wetu na kwamba nyenzo sahihi zinahitajika ili waweze kukabiliana na hali hii, lakini pamoja na yote hayo, tumejiridhisha pasipo shaka kwamba mradi huu wa Wema unahitaji kuchunguzwa kwa kina na kufuatiliwa kwa karibu na wadau mbalimbali wanaoguswa teknolojia husika,” inaongeza taarifa hiyo.

Taarifa hiyo inabainisha kuwa popote unapofanyika  barani Afrika, mradi huo umetawaliwa na usiri mkubwa.

Nyuma ya mradi wa WEMA tunaiona kampuni kubwa ya Monsanto ikiubeba utafiti huu, japo kuwa mradi huu unatekelezwa kwa ushirikiano wa sekta ya umma na sekta binafsi yaani Public Private Partnership baina ya African Agricultural Technology Foundation (AATF), ambapo wadau ni International Maize and Wheat Improvement Centre CIMMYT) Monsanto, na taasisi za kitaifa za utafiti wa kilimo kwenye nchi husika.

 

Tunajiuliza maswali mengi ni kwa namna gani mbegu za WEMA zitarekebisha mabadiliko ya tabia nchi? Hivi tunashindwa kubuni mbinu zitakazokabili tabia nchi na kumfanya mkulima wetu wa Afrika kutoingizwa kwenye mtego wa biashara ya mbegu za makumpuni ya nje?

 

Tunaushahidi bayana kuwa Monsanto ndiye aliyesambaza mbegu zilizobadilishwa vinasaba za mahindi zijulikanazo kama MON 810 kwa nchi nne zinazofanya majaribio ya WEMA ambazo ni Kenya, Msumbiji, Tanzania na Uganda, wakati aina hiyo hiyo imeripotiwa kufanya vibaya huko Afrika Kusini.

 

 

Asasi kwa kauli moja zinasema kwamba wakulima wa Kiafrika wanataka suluhisho la kweli na la kudumu juu ya mabadiliko ya tabia nchi, kinyume cha hapo mwendelezo wa tafiti za WEMA ni mbinu za makampuni makubwa kutaka kujimilikisha sekta ya mbegu barani Afrika na kuwafanya wakulima kubakia kuwa tegemezi wa mbegu huku faida kubwa itokanayo na biashara hiyo ikienda kwa makampuni hayo.

 

Mkutano huo wa wiki moja uliandaliwa na African Centre for Biodiversity (ACB) kwa kushirikiana na Kenya Biodiversity Coalition (KBioC), huku Tanzania ikiwakilishwa na